Xavi asaini kandarasi Barca sawa sawa na Howe huko Newcaste United

NA GODFREY NNKO

Klabu ya FC Barcelona na Newcastle United kila moja imeingia kandarasi na makocha ambao wanaamini wanakwenda kuwapa raha mashabiki wao.

Tuanzie kwa Barça au FC Barcelona kutoka katika Jiji la Barcelona nchini Hispania ambayo imekuwa ikifanya kweli katika La Liga, ipo hivi Xavi Hernande ambaye aliondoka miaka sita ndani ya klabu hiyo amepewa kandarasi ya kuinoa klabu hiyo.
Kocha Xavi. (Picha na FC Barcelona AP).

Hernandez kuanzia Novemba 8, 2021 ni mali halali ya Fc Barcelona baada ya kuhama kutoka Doha Qatar katika klabu ya Al Sadd akichukua mikoba ya Ronald Koeman ambaye alitimuliwa.

Xavi ametambulishwa katika dimba la Camp Nou mbele ya mashabiki 10,000 kufuatia kusaini mkataba utakaodumu hadi mwaka 2024.

Kocha Xavi amelazimika kuvunja mkataba na Al Sadd kwa kuilipa Pauni milioni 4.3 ili kurejea Camp Nou sehemu ambayo ilimtambulisha kwa kiasi kikubwa hadi kufikia hapo alipo.

Awali kocha huyo alipofika kuinoa Al-Sadd, aliapa siku moja kurejea kuifundisha klabu yake anayoipenda baada ya kujiandaa vyema kwa jukumu hilo.

Xavi anatajwa kuwa miongoni mwa makocha ambao wamekuwa na mafanikio makubwa kwa klabu ya Al-Sadd nchini Qatar, ndiyo maana FC Barcelona waliona kuna umuhimu wa kuharakisha mchakato wa kumrejesha ili aweze kuwasaidia kukabiliana na changamoto zinazoikabili klabu hiyo

Wakati hayo yakijiri huko mjini Newcastle upon Tyne nchini Uingereza, Klabu ya Newcastle United imevunja ukimya ambao ulitawaliwa na fununu za makocha wengi ambapo imempa kandarasi,Eddie Howe (43) aweze kuinoa klabu hiyo.
Kocha Howe. (Picha na Marca).

Kandarasi ya Howe kuinoa Newcastle United itadumu hadi mwaka 2024 ikiwa anachukua nafasi ya Steve Bruce aliyefukuzwa hivi karibuni.

Aidha, amekuwa nje ya kazi ya ukocha tangu alipoachana na Bournemouth mwishoni mwa msimu wa 2019-2020.

Howe mwanzoni mwa mwaka huu alifuatwa na vigogo wa Celtic ya Scotland, lakini alikataa kuridhia huku Newcastle ikitolewa nje na Unai Emery aliyesema anataka kubaki Villarreal ili kuipa makali zaidi.

Kocha huyo amekiri kuwa,hiyo ni heshima kubwa kuiongoxa klabu yenye historia kama Newcastle United na anajivunia jambo hilo katika maisha yake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news