DKT. BITEKO AFANYA MAAMUZI UCHENJUAJI BAHI

NA TITO MSELEM-WM

WAZIRI wa Madini,Dkt. Doto Biteko ameitaka Kampuni ya Uchenjuaji Madini ya dhahabu ya Binsulum Mine kuanza kufanya kazi ya uchenjuaji madini baada ya kukosa kibali cha mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kipindi cha miaka miwili tangu walipoomba.
Dkt. Biteko ametoa agizo hilo wilayani Bahi mkoa wa Dodoma mara baada ya kutembelea mgodi wa Binsulum Mine uliopo katika kijiji cha Nholi kata ya Mpalanga ambapo amesema ofisi yake itashirikiana na NEMC ili kibali cha mazingira cha Kampuni hiyo kipatikane haraka wakati kampuni hiyo ikiendelea na shughuli za uchenjuaji.

Aidha Dkt. Biteko amesema kuwa Serikali inampango wa kufanya utafiti na kuongeza Vituo vya Mfano vya Uchenjuaji madini katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo kuweka Kituo cha Mfano katika wilaya ya Bahi baada ya kuona uhitaji mkubwa wa mafunzo kwa wachimbaji wadogo.

Pia, Dkt. Biteko amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Mkunda kushirikiana na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma kutafuta eneo ili kifunguliwe Kituo cha kuuzia madini katika eneo la Nholi ili kuwapunguzia adha wachimbaji wadogo kwenda kuuzaia mbali madini yao.
Sambamba na hilo, Dkt. Biteko amewapongeza wachimbaji wadogo wa Nholi kwa juhudi za uzalishaji mkubwa wa madini ya dhahabu ambapo amesema zaidi ya asilimia 90 ya madini yote yanayouzwa katika Soko la Madini la Mkoa wa Dodoma yanatoka katika eneo hilo.

Pia, Dkt. Biteko ametumia fursa hiyo kuwaonya wote ambao bado wanatorosha madini na kuwataka wachimbaji wote kuwa walinzi wa rasilimali madini.

“Wapo baadhi ya Watu bado wanatorosha madini, mtu yoyote anayetorosha madini tumchukie tena ikibidi tuwaeleze Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwamba kuna mjanja mjanja anatorosha madini hapa ili wamfanyie kazi,” amesema Dkt. Biteko.

Vile vile, Dkt. Biteko amewataka wachimbaji wadogo wa madini wa Nholi kuhakikisha wanachimba kwa usalama na kuzingatia usalama mahali pa kazi ili kulinda afya za watu. 

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Bahi Shukrani Nollo ameeleza changamoto zilizopo katika eneo hilo na kumuomba Waziri Dkt. Biteko kuchangia ujenzi wa shule pamoja na Kituo cha Polisi katika eneo la Nholi ili watoto waweze kwnde shule na kusaidi ulinzi katika eneo hilo

Naye, Meneja wa mradi wa uchenjuaji dhahabu Mohamed Nassor amesema kuwa zaidi ya wafanyakazi 50 wamesimamishwa kazi kutoka na changamoto ya kukosekana kwa kibali kutoka NEMC ambapo Kampuni hiyo iliomba kibali hicho miaka miwili iliyopita.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news