Dkt.Grace Magembe atoa wito usimamizi miradi ya ujenzi wa EMD, ICU

NA ASILA TWAHA,OR-TAMISEMI

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya, Dkt. Grace Magembe amewataka wataalam wa afya kusimamia fedha zilizopekwa kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya Afya ikiwemo ujenzi wa EMD na ICU.
Akifungua kikao kazi cha kuwajengea uwezo Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri, Wahandisi wa Mikoa na Halmashauri na Waganga Wafawidhi wa hospitali zinazotekeleza miradi ya huduma za dharura na ICU leo Jijini Dodoma Dkt. Grace amesema kuwa, Serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi blilioni 236 kwa ajili ya miradi ya afya inayolenga kujikinga na athari za ugonjwa wa COVID -19 ikiwemo miradi ya ujenzi wa huduma za dharura (EMD) na ICU.

Ameendelea kufafanua fedha zilizotolewa ni pamoja na kujenga majengo ya huduma dharura 80, ununuzi wa vifaa tiba, ununuzi wa magari ya kubebea wagonjwa(ambulances) 195, ujenzi wa huduma ya hewa tiba ya oksijeni ambapo jumla ya oksijeni 5 zitajengwa katika maeneo matano ya kimkakati, kuimarisha huduma za X-Ray, ununuzi wa mashine 60 za X-Ray na ununuzi wa magari ya usimamizi wa huduma za afya.
Dkt. Grace amesema kikao hicho kitaleta manufaa kwa kuwakutanisha wataalam hao kwenda kushirikiana na kuleta ufanisi katika kusimamia na kutekeleza miradi ya ujenzi wa afya na huduma za dharura na ICU katika maeneo yao kwani lengo wananchi kupata huduma bora za afya.

“Kikao kazi hiki lengo ni tupate uelewa wa pamoja sababu sisi wote hapa ni wataalam hatutarajii kuona makosa yanatokea, twendeni tukashirikiane kwa pamoja kwa kusimamia na kutekeleza dhamana tuliyopewa ili tutoe huduma bora kwa wananchi,"amesema Dkt.Grace.

Aidha, amewashukuru wandaaji wa mafunzo wakiwemo Abbott Fund Tanzania kwa kushirikiana na Serikali kuhakikisha wanawaleta pamoja wataalam hao na kuhakikisha sekta Afya inaendelea kufikia malengo yake katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news