NA MWANDISHI MAALUM
SERIKALI ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imekusudia kujenga kilomita 150 za barabara kwa ajili ya miundombinu ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa anakudokeza mpango ulivyo hapa chini;
ii) Awamu ya Pili katika barabara za Kilwa, Chang'ombe, Kawawa hadi Magomeni na Sokoine ( KM 20.3),
iii) Awamu ya Tatu iko katika barabara ya Nyerere kutoka Gongo la Mboto hadi Makutano ya Bibi Titi na Ali Hasan Mwinyi na barabara ya Uhuru (Km 24.3);
iv) Awamu ya Nne iko katika barabara ya Ali Hasan Mwinyi na New Bagamoyo , kutoka Serena Hotel – hadi Tegeta na kutoka Mwenge hadi Ubungo (Km 30.1);
v) Awamu ya Tano ni barabara ya Mandela Kutoka Ubungo hadi Kurasini, na sehemu ya Barabara ya Tabata kutoka Segerea hadi Tabata Dampo (Km 27.6); na
vi) Awamu ya Sita ni kurefusha barabara zilizotajwa katika awamu ya kwanza, ya pili na ya nne (Km 26.6).