NA NTEGHENJWA HOSSEAH,OR-TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu amekagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Nata kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora na kuahidi kuletea vifaa tiba mara Kituo hicho kitakapokamilika.
Akitoa Taarifa ya Kituo hicho Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi wa kituo hicho Bw. Katunzi Jackson Kihembe amesema majengo yanayojengwa katika kituo hicho ni jengo la Wazazi, Upasuaji, Maabara na Jengo la wagonjwa wa nje.
Kituo cha Afya Nata kinategemewa kukamila January,2022 na kitatoa huduma kwa wakazi wa kazi ya Nata wapato 19,873.