Kiteto waja na mkakati wa kuongeza ufaulu kwa wanafunzi

NA MOHAMED HAMAD

SERIKALI wilayani Kiteto mkoani Manyara, imekuja na mpango wa kuongeza ufaulu wa wanafunzi kupitia mifumo mbalimbali ya kielektroniki.

Afisa Elimu Msingi Papakinyi Kaai akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri wilaya alisema Idara ya Elimu imejipanga vyema kuongeza ufaulu kwa wanafunzi shuleni.
Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Kiteto, Fadhili Alexander (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kiteto, John John Nchimbi, wakifuatilia kikao cha udhauri Wilaya ya Kiteto DCC.

Alisema, waratibu elimu kata wana kikao cha Online kupeana taarifa na uzoefu tofauti sambamba na kutatua changamoto za kielimu kwa wakati mara zinapojitokeza.

"Kwa vikao hivi Maafisa Elimu Kata wanapata uzoefu wa maeneo mengine na kupata uelewa wa pamoja na kwa wakati kwani inasaidia kuepuka gharama kubwa ya kuwasafirisha kwenda kwenye vikao," alisema Afisa Elimu huyo.

Alisema, katika mpango huo pia wanaangalia mahudhurio ya wanafunzi pamoja na walimu kila siku ya Alhamisi kupitia mtandao ambao nayo inasaidia kupunguza utoro na uzembe wa walimu katika ufundishaji.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kiteto John John Nchimbi akizungumza kwenye kikao cha Ushauri Kiteto DCC

"Katika wiki kunafanyika Tathmini ya ufundishaji kupitia mtaala wa elimu kwa kutumia fomu maalumu ambayo kila mwalimu anapitiwa kuangalia amefundisha vipindi vingapi kwa kila Kata kisha inakusanywa taarifa na kuunganishwa na Kata zingine kuunda taarifa ya Kilaya

Alisema, mifumo hiyo imechochea ufundishaji na Uwajibikaji Kwa walimu ambapo mpaka sasa ufaulu umefika asilimia 78.75 na mtihani wa kumaliza Elimu ya msingi ilikuwa asilimia 68.44 na darasa la nne la tatu na la sita matokeo yao bado.

Afisa Elimu huyo pia alisema katika hatua hiyo Idara imepata walimu wapya 36 ambapo wapo kazini isipokuwa mwalimu mmoja ambaye ni mtoro sugu ambaye amemuondolewa kwenye mfumo wa malipo.
Kutokana na taarifa hiyo Afisa Elimu huyo alisema matokeo hayo kwa asilimia kubwa hiyo hali ndio hali ya Elimu ilivyo Kiteto ambapo awali waalimu wa Sekondari wakilalamika kuwa Elimu Msingi wanawaletea watoto ambao hawajui KKK kidato cha kwanza lakini Kwa sasa walimu hao ndio wanasimamia mtihani wa msingi kumaliza darasa la saba na walimu wa msingi wanaenda kusimamia mtihani ya Sekondari.
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mbaraka Alhaj Batenga, akiongea na wajumbe wa kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Wilaya DCC mjini Kibaya.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mbaraka Al Haji Batenga, katika Kikao hicho alipongeza jitihada hizo akisema pia Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kupunguza adha ya wanafunzi kusomea chini ya miti na hata utoro.

Alisema, tafiti za Kiteto zilizofanyika kuhusu shule shikizi zimelisaidia Taifa kwa shule shikizi nyingi hapa nchini kuanza kupatiwa fedha baada ya taarifa hiyo ya Kiteto kuonyesha ukubwa wa tatizo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kiteto, Mohamed Kiyondo alipongeza Serikali Kwa kuongeza ufaulu kwa wanafunzi na kuiomba Serikali kuendelea kuondoa changamoto za kielimu zinazoendelea kujitokeza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news