NA GODFREY NNKO
MCHEZAJI wa zamani wa Ismaily na Kocha Mkuu wa Timu ya Al Magd inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Misri, Adham El Selhedar amefariki dunia baada ya timu yake kumaliza mchezo dhidi ya Al Zarka.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Desemba 2, 2021 katika dimba la Alexandria, Cairo nchini Misri wakati wakali hao wakiumana ambapo walipiga dakika tisi wakiwa na matokeo tasa.
El-Magd ya Alexandria walikuwa wanachuana na Al-Zarka katika siku ya tisa ya msimu wa mchezo ulionekana kuelekea sare tasa.
Vijana hao wa Alexandria, hata hivyo, walifanikiwa kupata bao la ushindi katika dakika ya 92 kupitia Mohamed Saad na kufanikiwa kupata alama tatu.
Wakati wa sherehe hizo, El-Selhedar alizimia ghafla na mara moja akakimbizwa hospitalini. Baadaye alifariki katika hospitali ya Al-Amriya huko Alexandria na ikabainika mshtuko wa moyo ndio sababu ya kifo chake.
Wakati wa uhai wake, El-Selhedar alitumia muda mwingi wa taaluma yake na Ismaily katika miaka ya 1990 na kufanikiwa kutwaa mataji ya Ligi Kuu na mengine mengi.
Tags
Michezo