Kuhani na Mwalimu Musa Richard Mwacha ampatia zawadi ya gari jipya linalotumia umeme, matufa Rose Muhando

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

KUHANI na Mwalimu Musa Richard Mwacha wa Ngome ya Yesu Kristo (Fresh Spring Fellowship) ya Kimara Temboni jijini Dar es Salaam amempatia zawadi ya gari jipya mwimbaji mkongwe na maarufu wa nyimbo za injili nchini, Rose Muhando.

Ngome ya Yesu Kristo ambayo huwakutanisha maelfu ya watu wa dini zote katika ibada za katikati ya wiki na Jumapili imezidi kuwa maarufu zaidi jijini Dar es Salaam kutokana na namna ambavyo watu wamekuwa wakipokea uponyaji wa papo kwa papo.

Rose Muhando ambaye alizaliwa mwaka 1976 katika Kijiji cha Dumila Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro licha ya kipawa alichonacho kwa ajili ya kumtumikia Mungu, amekuwa akipitia mapito mengi magumu ambayo mengine ni ya kukatisha tamaa na mengine ni ya kumpa nguvu ya kusonga mbele.

Awali, mama huyo alikuwa Mwisilamu na alikuwa ni mwimbaji mzuri sana wa kaswida na alihudhuria kila siku madrasa huko Dumila mkoani Morogoro.

Rose Muhando baadaye afya yake ilianza kudhoofu kutokana na ugonjwa ambao aliangaika kuupima ni ugonjwa gani, lakini hakukutwa na tatizo,hali hiyo ilipelekea maisha kuwa magumu sana.

Ndipo alipoamua kwenda kanisani kwenye maombi, baada ya maombi hayo, alipona na hapo ndipo alipoamua rasmi kubadili dini akiwa na umri wa miaka 12.

Kilichotokea,baada ya kubadili dini wazazi wake kuchukizwa na uamuzi wake,hivyo wakaona ni busara kumfukuza nyumbani kabisa.

Hali iliyozidi kuhatarisha maisha yake na kuendelea kutangatanga na kumsababisha aangukie mikononi mwa wanaume ambao alizaa nao watoto.

Akiwa na mtoto wa miezi sita jijini Arusha aliwahi kufukuzwa na mchungaji kisa alimuomba fedha ili aweze kuingia studio kurekodi kwa kipindi hicho mtoto alikuwa anaumwa ugonjwa wa pumu na alienda Arusha ili aweze kurekodi wimbo wake wa kwanza.

Alianza muziki rasmi katika kwaya iliyopo Dodoma, baadaye akawa mwalimu wa kwaya hiyo ya Dodoma St. Mary’s katika Kanisa la Kianglikana la Chimuli, aliendelea hivyo mpaka alipoamua kuanza kutunga nyimbo zake mwenyewe kwa msaada wa mfuko wa kwaya yao.

Mwana mama huyo ametwaa tuzo mbalimbali ambapo Januari mwaka 2005,alipokea tuzo mbalimbali ikiwamo ya Mtunzi Bora wa nyimbo za Injili, Mwimbaji Bora na Albamu Bora ya Mwaka, zilizotolewa na Tanzania Gospel Music Awards 2004,kupitia albamu yake ya Mteule uwe Macho.

Miongoni mwa albamu zake ni pamoja na Kitimutimu, Uwe Macho,Jipange Sawasawa,Utamu wa Yesu, Yesu Kun’guta na nyinginezo ambazo zimemfanya kuwa shujaa wa injili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news