Mabao matatu ya Simba SC dhidi ya Red Arrows waliyoyapata Dar yawavusha kwenda Makundi Kombe la Shirikisho barani Afrika

NA GODFREY NNKO

SIMBA SC wamefanikiwa kufuzu Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika licha ya kuchapwa mabao 2-1 na wenyeji, Red Arrows jioni ya leo Uwanja wa Taifa wa Mashujaa mjini Lusaka nchini Zambia.
Ricky Banda dakika ya 45 na Sadam Phiri dakika ya 48 wa Red Arrows ndiyo walioachia mabao kwao.

Aidha, Simba SC wamepata bao ambalo limefungwa na Hassan DIlunga dakika ya 67.

Simba SC inaingia hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 4-2 kufuatia kushinda 3-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam.
Ni katika mtanange ambao ulipigwa Novemba 28,2021 katika dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

Aidha,licha ya dimba kujaa maji siku hiyo, Simba SC ilicheza kandanda safi na kufanikiwa kuondoka mapumziko wakiwa na faida ya mabao mawili yaliyofungwa na Benard Morrison pamoja na Meddie Kagere.

Kipindi cha pili kilianza Simba SC ikionekana bado inahitaji magoli zaidi licha ya kuwa mbele kwa mabao mawili ambapo dakika 79 ilifanikiwa kupata bao la tatu kupitia tena kwa nyota wao Benard Morrison.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news