NA LUCAS RAPHAEL
MWANAMKE mmoja mkazi wa mkoani wa Arusha amekamatwa na Jeshi la Polisi katika stendi ya mabasi wilayani Sikonge mkoani Tabora kwa tuhuma za kukutwa na madini feki aina ya dhahabu waliyokuwa wakiwauzia wananchi wa kishrikiana na dereva wake.
Alibainisha kuwa, watuhumiwa walikamatwa baada ya kumtapeli mkazi huyo kiasi cha sh.340,000 ambapo pia baada ya kukaguliwa walikutwa na kadi tano za benki tofauti tofauti ambazo ni kadi za NMB 3, Posta 1na CRDB 1.
Vitu vinginevyo walivyokutwa navyo ni simu 4 aina ya iphone 6s plus, Tecno Spark 5 Air, Infinix hot 10 na Samsung zinazodhaniwa kuwa za wizi.
Aidha, ameongeza kuwa katika kukabiliana na matukio ya uhalifu, mauaji, unyang’anyi wa kutumia silaha, ujambazi na uvunjaji mkoani humo, jeshi hilo limeendelea kufanya operesheni mbalimbali katika wilaya zote.
Alitaja mafanikio ya operesheni hiyo kwa mwezi huu kuwa ni kukamatwa watu wawili, Khamis Baruti na Mohamed Shaban wakazi wa Izimbili wilayani Uyui kwa kukutwa na silaha aina ya gobore isiyo na namba za usajili iliyokuwa ikitumika kwenye uwindaji haramu.
Kamanda alitoa wito kwa wananchi wanazomiliki silaha kinyume na utaratibu kuendelea kuzisalimisha ndani ya kipindi hiki cha msamaha wa Waziri wa Ulinzi vinginevyo watakamatwa, aliitaka jamii kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa za vitendo vya uhalifu na wahalifu.