Mfumo mpya wa kielektroniki wa malipo ya ushuru wa maegesho ya magari warejesha faraja mitaani

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango wameboresha mfumo mpya wa Kielektroniki wa malipo ya Ushuru wa maegesho ya magari.
Kwa sasa kumbukumbu namba (Control number) itapatikana ndani ya dakika moja kwa kutumia njia ya Kutolewa Ankara kupitia kwa Mkusanya Ushuru, Kwa kutumia TeRMIS App (inayopatikana PlayStore),

Kwa kutumia GePG App (inayopatikana PlayStore & AppStore), kwa kutumia simu ya mkononi Piga *152*00# kisha fuata maelekezo na kwa kutumia wavuti ya mfumo inayopatikana kwa www.termis.tarura.go.tz.

Pia, TARURA imeboresha eneo la utoaji wa Elimu kwa kuanzisha Dawati la Malalamiko na kuweka namba za simu ambazo ni 0733-149658, 0733–149659 au 0733-149660 na kupitia namba hizi mteja atapiga simu na kutatuliwa changamoto yake. Pia anaweza kuwasilisha lalamiko lake katika Ofisi za TARURA zilizopo karibu yake.
Jinsi ya kulipia maegesho kwa kutumia simu ya mkononi

Piga *152*00#

1. Chagua 4 (Nishati, Madini na Usafiri)

2. Chagua 2 (TARURA)

3. Chagua 1 - Lipia Maegesho

4. Ingiza namba ya chombo cha Moto

5. Utapokea ujumbe mfupi

6. Bonyeza 1 Kuendelea

7. Ingiza namba ya Siri

8. Bonyeza 1 Kuthibitisha malipo ya Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news