NA MWANDISHI MAALUM
NAIBU Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Hussein Bashe (Mb) ameongoza kikao cha wataalam kutoka Wizara ya Kilimo pamoja na wawekezaji wa Kampuni ya Tree Global.
Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano Ofisi ndogo za Wizara, Kilimo IV Desemba 13, 2021 jijini Dodoma.

Mkutano huo una lengo la kuingia makubaliano kati ya Serikali na kampuni hiyo katika kupanda miti ya korosho na Cocoa kwa lengo la kutunza mazingira na kupunguza umaskini.

Katika kikao hicho, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Bw. Gregory Hess ameelezea jinsi ya matumizi ya teknologia katika ukuzaji wa mimea.