NA MWANDISHI DIRAMAKINI
MSEMAJI wa timu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire ameiomba Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kusaidia kubaini wahalifu walioanzisha ukurasa katika mtandao wa kijamii wa Twitter huku wakitumia jina lake na picha yake kupotosha Watanzania.
"Mkiona chochote kimeandikwa kwenye account yenye picha yangu hiyo, si mimi niliyeandika, ni wapuuzi fulani waliodhamiria kunichafua kwa upuuzi wao, wapuuzeni.
"Sijui TCRA, ni vipi wanaweza kunisaidia katika hili, polisi na vyombo vingine vya usalama...nisaidieni kukomesha upuuzi wa wapuuzi hawa ili, heshima yangu kwa jamii isiendelee kuchafuliwa na watu fulani kwa sababu wanazozijua wao.
"Kwa nini mtu/watu wanisemee nisichokifikiria, kukiwaza kukisema, kama ni chema, kwa nini wasijipambanue kwa majina yao wanibambike mimi kwa mchongo wao! Huu ni upuuzi,"ameeleza Masau Bwire.