Niara yatoa taulo za kike shuleni

NA HADIJA BAGASHA

TAKWIMU zinaonyesha siku 50 ndani ya mwaka mzima wanafunzi wa jinsia ya kike wanakosa vipindi vyao shuleni kutokana na changamoto ya hedhi.
Hayo yamesemwa na Veronica Mbilinyi ambaye ni Meneja mauzo kutoka kampuni ya Niara wakati wakifanya kampeni ya kuzunguka shuleni katika maeneo mbalimbali nchini na kuwagawia wanafunzi wa kike taulo za kike za "NIYA PADS" ili ziweze kuwasaidia pindi wanapokuwa katika hedhi.

NIYA Sanitary Pads zinatengengenezwa na kusambazwa na Kampuni ya Niara Co Ltd.
Meneja Veronica amesema kuwa, wameamua kufanya kampeni hiyo baada ya kuona kuna changamoto kubwa inawakabili mabinti wa kike kwa kuwagawia taulo za kike kwani baadhi yao wamekuwa wakikosa masomo yao na kukaa majumbani pindi wanapoingia kwenye hedhi.

"Lengo letu kama kampuni ya Niyara kuweza kutembelea baadhi ya mashule na kuweza kutoa taulo za kike kwa mabinti kwa sababu tumeona changamoto nyingi watoto wa kike wanazipitia, kampuni tumeamua kutoa kwa uchache taulo za kike katoni 10 kwa kila shule ambapo kila katoni inakuwa na pisi 24 na kufanya kila shule kupata pisi 240,"amesisitiza Veronica.

Meneja huyo amesema, kwa muda mfupi katika maeneo ambayo wameweza kuyatembelea wameona changamoto shuleni na kwamba watoto wengi wa kike wanashindwa kununua taulo za kike na hivyo kuwalazimu kukaa nyumbani na kukosa masomo yao ya kila siku na kusababisha ufaulu kushuka.

Sambamba na hayo ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa elimu sahihi ya matumizi ya taulo za kike ili kuwalinda mabinti na magonjwa mbalimbali yanayotokana na kukaa na taulo moja kwa muda mrefu ikiwemo magonjwa ya kansa ya kizazi, fangasi pamoja na UTI sugu.
Baadhi ya wanafunzi waliopatiwa msaada huo wa taulo za kike katika Shule ya Sekondari ya Istiqama iliyopo jijini Tanga wameishukuru kampuni hiyo na kusema kabla ya hapo walikuwa wakitumia vitambaa kujisitiri pamoja na taulo zisizokuwa na pamba, hali inayowalazimu kusoma kwa wasiwasi pindi wanapoingia kwenye hedhi.

"Tumefurahi sana kuletewa hizi zawadi sababu kabla ya hapo tulikuwa tukitumia taulo ambazo si rafiki na mazingira yetu ukizingatia shule yetu walimu wengi tuliokuwa nao ni wanaume kwa hiyo ikitutokea tatizo kama hilo inakuwa ni changamoto kwetu sisi wasichana,"amesema mmoja wa wanafunzi shuleni hapo.
Mmoja wa madaktari kutoka Hospitali ya Tanga Central jijini Tanga, Dkt.Sweetbertha Charles aliyeongozana na watendaji wa kampuni hiyo kwa ajili ya zoezi hilo la ugawaji wa taulo hizo amewataka mabinti hao pindi wanapokwenda madukani kwa ajili ya kununua taulo za kike kuhakikisha wananunua taulo ambazo zipo kwenye muda sahihi wa matumizi, kwani pindi watakapochukua zilizokwisha muda wake wanaweza kujisababishia madhara makubwa kiafya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news