VATICAN-Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis ameonya kuhusiana na ukimya wa Jumuiya ya Kimataifa juu ya masaibu wanayokabiliana nayo wananchi wa Mamlaka ya Palestina na huko Yemen.
Katika ujumbe wake wakati wa Sherehe ya Sikukuu ya Krismasi, Papa Francis ameonya kuhusu suala la migogoro kugeuka kuwa jambo la kawaida huku maelfu kwa maelfu wa wananchi wakizidi kuumia.
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis alipokuwa akiongoza misa ya Krismasi. (Picha na Getty Images).
Pia ametahadharisha kuhusu hatari ya kutokuwepo ushirikiano katika jumuiya ya Kimataifa, kukaa kimya na kutoguswa jamii ya kimataifa na mauaji ya kimbari na misiba mikubwa inayotokea katika maeneo mbalimbali duniani.
Hayo yanajiri wakati ambao Yemen, ambayo ni nchi masikini zaidi huko Mashariki ya Mbali, wananchi wake wanaelezwa kuwa na hali mbaya katika nyanja zote.
Machi 2015, Saudi Arabia pamoja na Umoja wa Falme za Kiarabu zikiwa zimepata idhini ya serikali ya Obama, zilianzisha vita vya pande zote dhidi ya wananchi waliodhulumiwa wa Yemen.
Wakati huo huo, Mamlaka ya Palestina, utawala wa Israel unatajwa kuendeleza sera zake za mauaji na ukandamizaji dhidi ya Wapalestina.
Aidha utawala huo unaendelea kukalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi na Quds (Jerusalem) ambapo Wapalestina wamekuwa wakitimuliwa kutoka ardhi zao za jadi.