Picha ya msanii wa Kimataifa,Rick Ross yafika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro

NA GODFREY NNKO

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limeendelea kutumia kila fursa inayojitokeza ndani na nje ya Tanzania kuhakikisha kuwa, wanatangaza vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini.
Picha ya msanii Rick Ross katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.(Picha zote na TANAPA).

Tanzania ni miongoni mwa Mataifa machache Duniani ambayo yana maeneo mengi ya vivutio vya utalii na vyenye sifa ya upekee.

Ni kuanzia milima mirefu, fukwe tulivu, misitu minene, hifadhi za taifa na hifadhi za ndege, visiwa na maeneo ya kale na ya kihistoria na mengine mengi bila kusahau ukarimu wa watu wake kunaendelea kuifanya Tanzania kuwa juu zaidi.

Aidha, jambo la faraja ni kwamba watu wanaopenda safari za kuvinjari wanaweza pia kufurahia matembezi ya kitalii kwenye misitu mbalimbali ya Tanzania.

Watalii wengi huwa wanapanga safari za mapumziko Tanzania kwa sababu ya amani, utulivu na ukimya wa nchi muda wote.

Upekee huo ndiyo unaoifanya Tanzania kupitia TANAPA mara nyingi kutwaa tuzo mbalimbali za Kimataifa ikiwemo tuzo ya kiwango cha dhahabu, ambacho ni kiwango cha juu kabisa cha ushindi duniani.

Washindi wa tuzo hiyo uchaguliwa kwa kuzingatia matokeo ya kura zilizopigwa, maoni ya wateja na utafiti wa masoko Duniani.

Matokeo hayo chanya huwa yanatokana na uongozi mahiri pamoja na ubunifu ndani ya TANAPA, kama ambayo wamemkaribisha mwanamuziki mashuhuri Duniani,Rick Ross kutembelea Mlima Kilimanjaro na Mbuga ya wanyama ya Serengeti.

Ni, kwa kupandisha picha ya msanii huyo katika kilele cha Mlima Kilimanjaro. 

Wachambuzi wa masuala ya mambo wameidokeza DIRAMAKINI BLOG kuwa, kwa wengine wanaweza kufikiri hilo ni tukio dogo. Lakini kimkakati, hiyo ni hatua kubwa.
Picha ya msanii Rick Ross katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Hivi karibuni Rick Ross alitamka anatamani kuja barani Afrika na kutembea Tanzania na kupanda Mlima Kilimanjaro pamoja na kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii
"Kongole kwa TANAPA, huu ni ubunifu mkubwa mno, endeleeni kubuni, mtayaona matokeo makubwa siku za karibuni, biashara ni matangazo na matangazo yenu mmeamua kutumia kinachojiri kufikisha ujumbe, safi sana,"amebainisha Mchambuzi katika mahojiano na DIRAMAKINI BLOG.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news