NA MWANDISHI DIRAMAKINI
VIOLETH Hassan Mtipa (32) ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Masweya Kata ya Mtunduru Wilaya ya Ikungi Singida amefariki dunia baada ya kupigwa na radi wakiwa wanazini na mume wa mtu kwenye jengo la Nyumba ambayo haijakamilika.
Katika tukio hilo la hivi karibuni, Violeth
alikuwa na mchepuko wake Hassan Nzige na wakati wanafikwa na majanga hayo walikuwa wakiendelea kufanya uzinzi huo.
Mmoja wa mahuhuda ameeleza kuwa, baada ya kupatwa na mkasa huo, Hassan Nzige alishindwa kusimama ndipo akaanza kupiga yowe kwa nguvu kwa ajili ya kuomba msaada, ndipo watu wakamkuta akiwa hajiwezi wakati mwenzake akiwa amepoteza maisha tayari.
Wanakijiji wa Masweya walimchukua Nzige aliyejeruhiwa miguu yake na kumkimbizwa zahanati ya Ndulungu, kwa matibabu ambapo inadaiwa kuwa kwa sasa anaendelea vema.
Saidi Hongoa amekiri kuwa tukio hilo lilitokea hivi karibuni majira ya jioni, muda mfupi kabla mvua haijaanza kunyesha.
Hongoa ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji Masweya amesema,radi ilipiga kabla ya mvua kuanza kunyesha.
"Wakati huo wakiwa kazini (wakizini) na wote wawili walikimbizwa katika zahanati ya Kijiji cha Ndurungu wakati mwanamke akiwa ameunguzwa vibaya shingoni na mgongoni na mwanaume alikuwa ameunguzwa miguuni, lakini walipofikishwa waliambiwa mwanamke alikuwa amepoteza maisha tayari,”amesema Mwenyekiti huyo.
Pia amesema, baada ya kutokea kwa tukio hilo, juhudi zilifanyika katika kumjulisha mume wake marehemu Violeth, Manase Nkungu aliyekuwa mbali na eneo hilo lakini aliposikia alilipokea kwa masikitiko makubwa taarifa hiyo.
Naye Diwani wa Kata ya Ndurungu, Theresia Daudi amsema, kuna kila dalili kwamba marehemu Violeth alifariki papo hapo kwa vile aliunguzwa sehemu nyeti za mwili wake japo ni vigumu kueleza.
Mume wa marehemu, Manase Nkungu akiwa na masikitiko amesema hakutegemea kuwa angepata pigo kubwa la ghafla namna hiyo katika kipindi ambacho alimwamini mkewe, Violeth.
Amesema, mkewe Violeth amemwachia watoto wanne hivyo inampa wakati mgumu wa namna gani anavyoweza kujipanga kwa namna ya kuwalea na kuwajenga kisaikolojia kwa sasa.