NA GODFREY NNKO
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba Mosi, 2021 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said walioteuliwa na Mheshimiwa Rais ni viongozi wanne.
Miongoni mwa viongozi hao ni ndugu Said Haji Mdungi ambaye, Mheshimiwa Rais Dkt. Mwinyi amemteua kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Nishati na Madini katika Wizara ya Maji na Nishati na Madini Zanzibar.
Pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Meja Jenerali mstaafu Sharif Shehe Othman kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO).
Aidha, uteuzi wa tatu, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Meja Jenerali mstaafu Said Shaaban Omar kuwa Mwenyekiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA).
Uteuzi wa nne, Mheshimiwa Rais Dkt. Mwinyi amemteua, Meja Jenerali mstaafu Issa Suleiman Nassor kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA).
Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa hiyo,Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said, uteuzi huo umeanza leo Desemba Mosi, 2021.