NA MWANDISHI DIRAMAKINI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewaapisha Wajumbe wapya wa Tume ya Mipango ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mwanasheria Mkuu, Mhe.Dkt. Mwinyi Talib Haji, kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango, hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Hafla hiyo imefanyika leo Ikulu jijini Zanzibar ikiwa ni kikao
cha kwanza cha tume hiyo katika Awamu ya Nane ya uongozi wa Rais Dkt.
Mwinyi ambapo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman
na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah
walishiriki ikiwa ni Wajumbe kutokana na vyeo vyao.
Mara baada
ya kiapo hicho, Rais Dkt. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuwapongeza Wajumbe
hao wapya aliowaapisha pamoja na wale wa zamani wanaoendelea.
Katika
pongezi hizo, Rais Dkt. Mwinyi alieleza matumaini yake makubwa kwa
wajumbe hao wa Tume ya Mipango ya Zanzibar katika kufikia malengo
yaliyokusudiwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar,Mhe Jamal Kassim Ali,kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango,hafla hiyo imefanyika leo katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akisaini hati ya Kiapo ya Waziri wa Ardhi, Maendeleo na Makazi Zanzibar, Mhe.Riziki Pembe Juma, baada ya kumuapisha kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango, hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mhe. Omar Said Shaban, kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Wajumbe walioapishwa ni Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu
Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar
Dkt. Mwinyi Talib Haji,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango
Jamal Kassim Ali, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Riziki Pembe
Juma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mudrik
Ramadhan Soraga.
Wengine ni Waziri wa Biashara na Maendeleo ya
Viwanda Omar Said Shaaban,Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi
Rahma Kassim Ali, Waziri wa Maji, Nishati na Madini Suleiman Masoud
Makame,Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Lela Muhamed Mussa, Waziri wa
Uchumi wa Buluu na Uvuvi Abdalla Hussein Kombo pamoja na Dk. Rahma Salim
Mahfoudh Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Zanzibar, Mhe. Rahma Kassim Ali, kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Waziri wa Uchumu wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Abdalla Hussein Kombo,kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango.
Wajumbe hao wapya walioapishwa leo wameahidi kutekeleza majukumu yao kwa maslahi na uchumi wa Zanzibar.
Nao wajumbe wa zamani wa Tume hiyo ya Mipango ya Zanzibar Mohammed Faki Mohammed pamoja na Profesa Semboja Haji Hatib walitoa shukurani zao kwa Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi kwa kuendelea kuwaamini kuwa Wajumbe wa Tume hiyo na kuahidi kwamba wataendelea kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar.