NA MWANDISHI DIRAMAKINI
JARIDA la Forbes Africa limemtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa miongoni mwa wanawake 100 wenye nguvu Duniani.
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Awamu ya Sita wa Tanzania ambaye aliingia madarakani Machi,2021 baada ya kifo cha mtangulizi wake, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania toka mwaka 2015.
Rais Samia ameweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo wa juu zaidi nchini Tanzania.
Pia ni rais wa pili wa Tanzania kutokea Zanzibar, wa kwanza akiwa Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyeliiongoza Tanzania kwa miaka 10 kutoka mwaka 1985 mpaka 1995.