Serikali yakemea vitendo vya kuchangisha wazee michango wilayani Karatu

NA SOPHIA FUNDO

SERIKALI wilayani Karatu mkoani Arusha imelaani vitendo vya baadhi ya viongozi wa vijiji kuwachangisha michango wazee wenye umri zaidi ya miaka 60 na kuwatoza faini pale wanaposhindwa kulipa michango hiyo.
Viongozi wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha wakipokea maadamanao ya halaiki kutoka Shule ya Msingi Bwawani katika kilele cha Maadimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Kauli hiyo imetolewa Desemba 9,2021 na Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Faraja Msigwa aliyemwakilisha mkuu wa wilaya katika kilele cha maadimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Bi.Msigwa amesema kuwa, wazee hao ndio waliopigania Uhuru wa Tanzania na leo hii tunasherehekea kwa heshima yao, hivyo hatuna budi kuwapa heshima yao na kuwatatulia changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Pia aliwaagiza watendaji kuwapa ushirikiana wazee katika maeneo yao kwa kuyashirikisha mabaraza ya wazee katika vikao ili washiriki katika maamuzi yanayotolewa na kata.

Katika risala yao wazee walieleza changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo wazee kutoshirikishwa katika maamuzi ya kata pamoja na wazee kupata shida katika kupata huduma ya afya kwa kigezo cha kufuata barua mara kwa mara ofisi za kata kwa kukosa bima ya afya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu mkoani Arusha,Karia Magori (katikati) walioshika mfano wa hundi pembeni mwake ni Mwenyekiti wa halmshauri hiyo,John Lusian na Katibu Tawala, Faraja Msigwa wakikabidhi hundi hiyo vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.

Akizungumza katika maadimisho hayo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Karia Magori aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa viongozi wa ngazi zote katika kutimiza malengo ya serikali ya kuendeleza yale yote yaliyoanzishwa na waasisi wa Tanzania kwa kutekeleza miradi mbalimbali iliyotengewa fedha na serikali.

Katika maadhimisho hayo halmashauri ya wilaya imewakabidhi mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 170 vikundi mbalimbali vya vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news