Serikali yatoa tamko rasmi kuhusu wananchi kupata dalili za mafua

NA GODFREY NNKO

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewatoa wasiwasi wananchi kuhusu ongezeko la wengi kupata dalili za mafuta ya kawaida.

"Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii, kumekuwa na taarifa zenye kuonesha kuwa watu wengi wana dalili za kukohoa, mafua, maumivu ya mwili na kuchoka, Wizara imefuatilia na kubaini kweli kuna ongezeko la Wananchi kupata dalili za mafua;
"Hata hivyo, hii huwa ni hali ya kawaida kila mwaka (seasonal influenza) ambayo huchangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa kama ambavyo iliweza kushuhudiwa kwa miaka mingine iliyopita, hata hivyo, Wizara na taasisi zake tunaendelea kufuatilia kwa karibu viashiria vya mwenendo wa hali hii;

"Aidha, Wizara inashauri kuwa wananchi wenye dalili hizi za kukohoa, mafua, maumivu ya mwili na kuchoka watoe taarifa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili wafanyiwe uchunguzi wa kitaalamu na wapatiwe matibabu stahiki.

"Pamoja na hali hii ya mwenendo wa mafua ya kawaida, vilevile Wizara inaendelea kukumbusha na kutoa tahadhari kwa kila Mtu kuendelea kuchukua hatua zote muhimu za kujikinga na janga la UVIKO-19 ikiwa ni pamoja kuepuka misongamano isiyokuwa ya lazima, kunawa mikono, kuvaa barakoa na kuhakikisha kuwa kila Mtu anapata dozi kamili ya chanjo.

"Wito kwa wananchi kutoa taarifa za tetesi za viashiria vya magonjwa ya mlipuko kutoka katika jamii kupitia namba ya simu 199 bila malipo yoyote,"ameeleza Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt.Aifello Sichalwe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news