NA HADIJA BAGASHA
JITIHADA za haraka zimetakiwa kufanyika ili kukabiliana na shughuli za kilimo na uchimbaji wa madini unaofanywa kwenye vyanzo vya maji vya Mto Zigi ambao ni tegmeo la wakazi wa jiji la Tanga na maeneo mengine ya mkoa wa Tanga.
Wadau wa jukwaa hilo wamezungumzia uharibifu wa vyanzo vya maji vya Mto Zigi, uharibifu unaotokana na shughuli za kibinadamu ikiwemo uchimbaji wa madini.
Abrahamu Isaya ni kaimu mkurugenzi bodi ya maji Bonde la Mto Pangani amesema kwamba, changamoto walizokuwa nazo katika usimamizi wa rasilimali za maji kuwa bado ni kubwa ukilinganisha na mafanikio ambayo wameyapata.
“Kiukweli tumefanikiwa katika eneo kubwa lakini tunaendelea kuongeza jitihada ndio maana leo hii tumekaa kikao kazi cha pili kwajili ya kuhakikisha kwamba lengo la serikali la kusimamia rasilimali za maji zinakuwa endelevu,”alisisitiza Issaya.
Naye Rosemery Rwebugisa ni kaimu Mkurugenzi Wizara ya Maji, idara ya Rasilimali Maji amesema kwamba hivi karibuni wameona kuna changamoto ya uharibifu wa vyanzo vya maji kutokana na uvamizi wa jamii kwajili ya kufanya shughuli za kimaendeleo ikiwemo kilimo,mifugo,na hata ufyatuaji wa matofali sambamba na kumwaga maji taka kwenye vyanzo hivyo.
“Hizi jumuiya zinapoanza kukusanya fedha na zikawa na fedha kwao inakuwa ni mtihani leo tumekaa wenyewe, lakini mkipata fursa siku moja tokeni nendeni mkakae na hizo jumuiya kwenye mikutano yao mtajifunza kitu moja ya kitu ambacho kipo wanakusanya fedha nyingi mwisho wa siku fedha hizi wanazitumia ovyo,”amesisitiza DC Mgandilwa.
Mto Zigi ndio mto pekee unaotegemewa na wakazi wa Wilaya ya Tanga na kwamba kama shughhuli za kibinadamu zitaendelea kushamiri kwenye mto huo upo uwezekano wa jiji la Tanga kuingia kwenye shida ya maji.