Tanzania yaanza kufuatilia madai ya uwepo wa kirusi cha Omicron

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

SERIKALI ya Tanzania imesema tayari imeanza kufuatilia kupitia vyombo vya ndani taarifa za uwepo wa abiria mmoja aliyerudi nyumbani nchini India mwenye aina mpya ya kirusi cha UVIKO-19 cha Omicron ambaye alitokea hapa nchini.
Picha na Getty Images.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Abel Makubi ameyasema hayo Desemba 5,2021 wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Mazungumzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam yaliangazia kuhusu ufafanuzi wa abiria huyo na wito wa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya UVIKO-19.

Profesa Makubi amesema, kwa kushirikiana ubalozi wa Tanzania nchini India wanafuatilia ili kubaini ukweli wa jambo hilo na baadaye kuchukua hatua stahiki.

“Bado haijajulikana kama abiria huyu alitokea Tanzania moja kwa moja au alipita Tanzania kuelekea India. Pia haijulikania alipita wapi kabla ya kufika India,” amesema Profesa Makubi.

Amesema, Maabara ya Taifa pia imekuwa ikichunguza mabadiliko ya kirusi kwa kuangalia uwepo wa anuwahi mbalimbali zinazotokana na mabadiliko ya UVIKO-19 ikiwemo anuwai mpya ya Omicron.

Amesema, maabara inao uwezo wa kubaini anuwai mpya ya Omicron na wanaendelea kuzifuatitilia sampuli zote na kwamba wakibaini uwepo wa anuwahi mpya watatoa taarifa.

“Mpaka sasa uchunguzi zaidi ya wanasayansi duniani unaendelea kujua anuai hii ya Omicron ina madhara ya kiasi gani kwa mtu anapoambukizwa na taarifa kutoka mataifa yaliyobaini wananchi wenye virusi hivi, wamekuwa na dalili za kiasi na nyepesi bila kuingia mahututi,” amesema.

Pia amesema waliobainika wengi wamechanja hivyo huenda chanjo imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza makali ya ugonjwa.

Profesa Makubi amewasihi wananchi kutokuwa na hofu kutokana na habari hiyo bali waendelee kuwa watulivu na kutekeleza shughuli za maendeleo huku wakichukua tahadhali zote ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka, kuvaa barakoa na kujiepusha na misongamano isiyokuwa ya lazima na kufuata miongozo mbalimbali inayotolewa na wizara kupambana na UVIKO-19 nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news