Dada wa marehemu, Asha Zahor, alisema kaka yake amefariki dunia saa tatu asubuhi baada ya kusumbuliwa na maradhi mbalimbali.
Alisema,kabla ya umauti, marehemu Zahoro alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kisukari na shinikizo la damu kwa muda mrefu.
“Amefariki akiwa anaendelea na matibabu, tulitoka hospitali baada ya kusumbuliwa kwa maradhi muda mrefu, tukarudi nyumbani ilipofika saa tatu asubuhi alifariki,” alisema kwa majonzi.
Dada huyo wa marehemu alieleza kuwa, msiba upo Chanika nyumbani na maziko yatafanyika katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam saa 10.00 alasiri.
Alieleza kuwa, Zahoro alikuwa ni mtoto wa pili na baada ya mtoto wa kwanza kufariki ndio alikuwa mkubwa wa familia yao yenye watoto tisa kwa Baba na mama mmoja.
Aliongeza kuwa baba wa Zahoro alishafariki dunia na walibaki na mama mzazi, hivyo Zahoror amefariki akiwa amemwacha mama yake mzazi na nduguze saba.
Zahoro alianza kwa kuandika hadithi katika magazeti ya Uhuru, akiwa mwandishi wa kujitegemea mnamo mwaka 1995 aliajiriwa rasmi na kuanza kuitumikia taasisi hiyo.