MRADI wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Julius Nyerere (JNHPP-MW2115) ujenzi wake umeendelea kushika kasi kutokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Kukamilika kwa mradi huo kutafanya Tanzania kuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 4478 pamoja na vyanzo vingine vya umeme vilivyopo huku mahitaji yakiwa ni megawati 2788 na hivyo kufanya kuwa na ziada ya umeme wa megawai 2100.