NA MWANDISHI MAALUM
WAZIRI wa Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed O. Mchengerwa kwa kushirikiana na wasaidizi wake katika wizara hiyo wamepongezwa kwa juhudi na maarifa ambayo yameonyesha wazi kuwa wanamsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kusongesha gurudumu la maendeleo kuanzia wizarani na Taifa kwa ujumla.
"Hongera Waziri Mchengerwa kwa kumsaidia vema Mhe. Rais kutetea na kuhimiza masilahi ya Watumishi wa Umma-Steven Sabiano.
Mojawapo ya majukumu ya wizara hiyo ni kusimamia misingi yote ya Utumishi kwa kulinda maadili ya Utumishi wa Umma nchini.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazosimamia utawala bora, hivyo Serikali ikaona umuhimu wa uwepo wa Wizara hiyo ambayo ipo chini ya usimamizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.