NA MWANDISHI MAALUM
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ameibuka kidedea mashindano ya Gofu ya Wabunge ya Afrika Mashariki kwa ushindi wa jumla upande wa Wabunge Wanaume akiwakilisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri Dkt. Ndumbaro amekuwa kinara kwa kupata pointi 73 huku akiwaacha washindani wake kwa kiasi kubwa.
Akielezea ushindi huo, Dkt. Ndumbaro amesema kuwa, uzoefu na kufanya mazoezi mara kwa mara vimeweza kumbeba kwa kuibuka mshindi katika mashinadano hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa mchezaji mwenzake wakielekea kupiga shimo la 18 katika Mashindano ya Gofu ya Mabunge ya Afrika Mashariki 2021, yanayofanyika katika uwanja wa mchezo huo wa Kili Golf uliopo Usa River jijini Arusha ambapo kwa timu ya wanaume ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Ndumbaro ameibuka kuwa mshindi wa jumla kwa wanaume kwa kujipatia pointi 73.
"Mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa, Kila mmoja wetu alijipanga kuwa mshindi lakini matokeo mazuri yamekuja Tanzania, Siri ya ushindi wangu ni uzoefu wa mazoezi ninayofanya mara kwa mara,"amesema Waziri Dkt. Ndumbaro.
Katika matokeo hayo ya Mabunge Waziri Dkt. Ndumbaro ameibuka mshindi wa jumla katika mashindano hayo.
Mashindano ya Gofu ya Mabunge ya Afrika Mashariki 2021, yanafanyika katika uwanja wa mchezo huo wa Kili Golf uliopo Usa River jijini hapa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa amepiga mpira wakati wa Mashindano ya Gofu ya Mabunge ya Afrika Mashariki 2021, yanayofanyika katika uwanja wa mchezo huo wa Kili Golf uliopo Usa River jijini Arusha ambapo kwa timu ya wanaume ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Ndumbaro ameibuka kuwa mshindi wa jumla kwa wanaume kwa kujipatia pointi 73.
Mbali na mashindano ya gofu katika Jiji hilo pia kuna mashindano mengine ya Mabunge ya Afrika Mashariki yanayoendelea kufanyika katika viwanja mbalimbali jijini hapa.
Bunge la Tanzania liliweza kujikusanyia ushindi wa jumla ya pointi 43.5, huku Kenya ikipata pointi 37, Uganda pointi 35.8 na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ( EALA) waliibuka na ushindi wa pointi 17.7.
Kipengele cha Wabunge Wanaume ushindi wa jumla ulienda kwa Waziri Dkt. Ndumbaro akiwakilisha Tanzania kwa kunyakuwa pointi 73 huku ushindi wa Wabunge wanawake Mhe. Neema Mgaya (Tanzania), yeye alipata pointi za jumla 48 zilizompa ushindi upande huo.
Aidha, washindi wengine kwa Wanawake ni Uganda ilipata pointi 36.2 na Tanzania ikapata pointi 31.5, Kenya wao walipata pointi 20 huku Bunge la Afrika Mashariki ( EALA ) likiibuka la mwisho kwa pointi 16.6.
Ushindi mwingine kwa upande wa Wabunge wa Bunge la Tanzania upande Wanaume walipata pointi 51.3, Kenya pointi 44.3,Uganda wao pointi 35.4 na kwa Bunge la EALA nao waliibuka na ushindi wa pointi 19.6.