Waziri Mkuu wa Uingereza apata mtoto wa kike Siku ya Uhuru wa Tanzania Bara walioupata kutoka kwao

NA GODFREY NNKO

MKE wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, Bi. Carrie amejifungua mtoto wa kike katika Hospitali Kuu jijini London.
Waziri Mkuu wa Uingereza,Boris Johnson na mkewe Bi. Carrie Johnson wakati wa Mkutano wa G7 huko Cornwall, England mwezi Juni. (Getty Images file).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa familia hiyo, Bi.Carrie amejifungua mapema asubuhi ya Alhamisi ya Desemba 9,2021.

Siku ambayo pia Tanganyika ilikuwa inasherehekea na kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru walioupata kutoka kwa Koloni la Uingereza Desemba 9,1961.

“Wote, mama na binti wapo salama. Familia hii inapenda kutoa pongezi za pekee kwa wahudumu wa NHS kwa usaidizi wao na uangalizi,"Msemaji wa Familia amebainisha.

Huyu ni mtoto wa pili kwa wanandoa hao, baada ya mzaliwa wa kwanza wa kiume, Alfred aliyezaliwa Aprili 2020, wawili hao walifunga ndoa mwezi Mei mwaka huu.

Mheshimiwa Johnson, kabla alikuwa ameoa mara mbili huku akiwa hapendi kuweka wazi idadi ya watoto waliozaa.

Aidha,alikuwa na watoto wanne na mke wake wa pili, Marina Wheeler, wakili.

Mheshimiwa Johnson, alipata habari za furaha ikiwa ni siku moja baada ya kupata shinikizo la kuelezea ripoti kwamba wafanyakazi wake mwaka jana walifanya Sherehe ya Krismasi ambayo ilikiuka sheria za Mapambano Dhidi ya Uviko-19 za nchi hiyo, wakati kesi zilikuwa zikiongezeka na watu kote nchini walipigwa marufuku kufanya aina nyingi za mikusanyiko.

Pia aliamuru uchunguzi ufanyike Jumatano na akasema alikuwa na hasira kuhusu hali hiyo.

Historia ya Uhuru

Historia ya Tanzania Bara ilianza na wakoloni wa Ulaya. Karne ya 18 ilikuwa na dola ndogo za miji katika mwambao baada ya kukaliwa na waarabu kutoka Oman. 

Ilikuwa karne 7 baadae mwaka 1499 wakati baharia wa Kireno Vasco da Gama alipotembela visiwa vya Zanzibar. 

Baada ya takribani miaka 100 au kabla ya karne ya 16 Wareno waliichukua Zanzibar. Wareno hawakukaa muda mrefu sana na mwaka 1699 walipinduliwa na waarabu wa Oman waliorudi kuitawala Zanzibar. 

Kwa hiyo katika karne ya 18 Sultan wa Oman aliimarisha utawala wa waarabu katika mwambao wa Afrika Mashariki na kuufanya uwe sehemu ya Zanzibar.

Mwaka 1840 wakati Sultan Seyyid bin Sultan alipohamisha mji wake mkuu kutoka Oman kuja Zanzibar, biashara ya utumwa na pembe za ndovu ilistawi. 

Mwaka 1861 utawala wa Sultan wa Zanzibar na Oman ulitengana baada ya kifo cha Seyyid. Katika karne ya 19 wazungu walianza kuvumbua bara, wakafuatiliwa kwa karibu na wamishionari wa kikristo. 

Mwaka 1884 German Colonization Society ilianza kutoa ardhi bara kwa kuipinga Zanzibar na mwaka 1890 Uingereza ilichukua hadhi ya kuilinda Zanzibar, ikakomesha biashara ya utumwa na kutambua madai ya Ujerumani kwa bara. German East Africa ilianzishwa rasmi kama koloni mwa 1897.

Mwaka 1905-1907 Vita ya Majimaji ilizimwa kikatili na majeshi ya kijerumani. Matukio ya duniani yakajitokeza kwa kutokea Vita vya Kwanza vya Dunia, na kama ilivyokuwa huko Ulaya, German East Africa haikukwepa vita hivyo, ingawa vita vikali havikuchukua muda mrefu kutokana na kushindwa kwa German East Africa na Waingereza 1916. 

Mwaka 1919 iliyokuwa Umoja wa Mataifa ndio iliipa Uingereza mamlaka kutawala sehemu ya German East Africa aliyojulikana kama Tanganyika. Mwaka 1946 Tanganyika ilikuwa nchi iliyo chini ya udhamini wa Umoja wa Mataifa.

Baraza la kutunga sheria liliundwa mwaka 1926, likaongezwa mwaka 1945 na kuundwa upya mwaka 1955 na kutoa uwakilishi sawa kwa waafrika, waasia na wazungu, kuwa na viti 30 vya wasio rasmi na 31 walio rasmi. 

Mwaka 1954 Mwalimu Julius Nyerere alianzisha chama cha Tanganyika African National Union (TANU) kilichohimiza utaifa wa waafrika na kuleta mabadiliko ya katiba ya kuongeza sauti ya waafrika na kutenga viti kwa ajili ya jumuiya ndogondogo.

Uchaguzi ulifanyika mwaka 1958 na 1960. Matokeo ni ushindi mkubwa kwa TANU ambayo wakati huo ilikuwa ikifanya kampeni kubwa kwa ajili ya uhuru pamoja na utawala wa wengi. Serikali mpya na serikali ya Uingereza walikubaliana katika mkutano wa katiba mjini Uingereza kuipa Tanganyika uhuru kamili Desemba 1961. Hadi Desemba 9,2021 Tanzania Bara imetimiza miaka 60 ya Uhuru. (Mashirika)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news