NA MWANDISHI DIRAMAKINI
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Ummy Mwalimu ameongeza siku 15 kwa halmashauri zote nchini kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Kutokana na uamuzi huo,kwa sasa vyumba vyote vya madarasa vitakabidhiwa Desemba 31, 2021 badala ya Desemba 15,2021 kama ilivyoelekezwa hapo awali.