Waziri Ummy ashuhudia matunda ya fedha za tozo za miamala ya simu wilayani Handeni

NA RAPHAEL KILAPILO

HALMASHAURI ya Mji wa Handeni, Tanga imepongezwa kwa kutekeleza ujenzi wa vituo vya Afya kupitia fedha za tozo ya miamala ya simu kwa weledi mkubwa unaoanza kuonesha matunda ya tozo hizo.
Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) alipotembelea Halmashauri ya Mji wa Handeni mkoani Tanga kukagua miradi ya maendeleo.

“Nimefurahi kukuta pesa za tozo za miamala ya simu zimeanza kutumika vizuri mmejenga kituo cha afya Malezi ambacho mmeniambia mmefikia asilimia 75 ambapo kitakapokamilika kitahudumia zaidi ya wakazi 10000 wakiwemo wananchi wa kata za jirani. Hongereni sana,"alisema Ummy.
Mheshimiwa Ummy alieleza kuwa, Oktoba 10, 2021 Serikali ilitoa shilingi milioni 260 kwa kila jimbo kujenga vituo vya Afya kutokana na fedha za tozo ya miamala ya simu, lakini anashangazwa kuona watu hawaziongelei ili wananchi waone matunda yake.

“Nimefurahi sana mmenileta hapa kuona kazi inavyoendelea ya kujenga Kituo hiki cha Afya kinachotokana na fedha za Tozo. Hongereni sana, nimeridhika na hatua ya ujenzi,"alisema Ummy.
Aidha, aliwataka viongozi wote wa halmaashauri nchini kuendelea kusimamia fedha hizo kwa umakini mkubwa na kuhakikisha fedha hizo zinawaletea matunda wananchi na kuwapunguzia machungu ya kwenda mbali kufuata huduma za afya.
“Nichue fursa hii kuwataka wakurugenzi wote ambao walipata Milioni 250 za kujenga vituo hivi vya Afya, ambao wanefika zaidi ya asilimia 70 waombe tena milioni 250 ili kukamilisha milioni 500 zilizotolewa na wananchi wafurahie matunda ya Serikali yao ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan,"alisema Ummy.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news