NA ATLEY KUNI, WAMJW
KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Prof. Abel Makubi, amesema kuelekea uzinduzi wa Kampeni Harakishi na Shirikishi awamu ya pili, itakuwa ni kampeni ya Mtaa kwa Mtaa na Nyumba kwa nyumba wakiwatumia watoa huduma ngazi ya jamii zaidi 8,130 waliopatiwa mafunzo ya namna bora yakuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa chanjo katika kukabiliana na Uviko-19 kisha mwananchi kuchukua hatua yakuchanja ridha yao.
Akizungumza na waandshi wa Habari hivi leo Desemba 19, 2021 jijini Dodoma, Prof. Makubi amesema, Mpango Shirikishi na Harakishi awamu ya pili wa mapambano dhidi ya UVIKO-19, tayari wameshan zielekeza timu za afya za Mikoa na Halmashauri, kuendelea kuwatumia Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii, Viongozi wa Dini Kimila sambamba Pamoja na makundi yote yenye ushawishi ndani ya Jamii.
Prof. Makubi amesema ajenda hiyo ya Kampeni Shirikishi na harakishi ina sura ya kitaifa kwa Wizara zote za kisekta, aidha kwakutambua hilo, tayari Ofisi ya Rais-TAMISEMI, imeandaa Mwongozo wa Wawezeshaji na Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii ikiwa ni pamoja na kuwatambua Wahudumu waliopo katika ngazi ya Vijiji, Mitaa na Vitongoji na kuanza kuwajengea uwezo kwa kuwapatia mafunzo kuhusu afua za kinga dhidi ya UVIKO - 19 na umuhimu wa wananchi kuchanja.
Prof. Makubi ameongeza kuwa, kwakuwa vita hivyo ni vya kila mtanzania basi hata kundi la wanahabari, halinabudi kuwa mstari wa mbele kuhamasisha ili kuwezesha kufanikisha kampeni hiyo itakayozinduliwa mkoani Arusha.
Serikali inategemea wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo mkoani Arusha Desemba 22, 2021, uwepo wa baadhi ya Wakuu wa Mikoa, Wizara mbalimbali za kisekta, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Mitaa, Taasisi za binafsi, Wadau wa Maendeleo, Viongozi wa Siasa kama Wabunge, Madiwani, Wamiliki wa Vyombo vya Usafiri, Makapuni ya Simu na Wanahabari.
Serikali ya Tanzania ilianza kutoa chanjo za UVIKO-19 mapema mwezi Agosti, 2021, huku chanjo ya Jenssen ikiwa ndio chanjo ya awali kabisa kutolewa na kufuatiwa na Sinopharm na Pfizer zenye dozi mbili kwa kila chanjo, aidha hadi kufikia tahehe 18 Desemba, 2021 jumla ya wananchi wapatao 1,275,795 walikuwa, wamejitokeza na kupata chanjo kamili na kupata kinga kamili dhidi ya UVIKO-19.