NA MWANDISHI DIRAMAKINI
UONGOZI wa Azam FC umeingia mkataba wa miaka mitatu na Omar Abdikarim Nasser kuwa Kocha Msaidizi mpya.
Ujio wa Nasser aliyesaini mkataba mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', ni sehemu ya mapendekezo ya Kocha Mkuu, Abdihamid Moallin.
Nasser amewahi kufanya kazi katika nchi mbalimbali, mara ya mwisho 2019, akiitumikia moja ya vigogo vya nchini Qatar, Al Sadd, akiwa kama mchambuzi wa mechi (analyst) kabla ya kufanya majukumu kama hayo akiwa Al Duhail ya huko pia.
Al Sadd ni moja ya timu kubwa nchini humo, iliyokuwa ikinolewa na gwiji wa zamani wa Hispania, Xavi Hernandez, kabla kurejea Barcelona, akiwa kama Kocha Mkuu.
Tags
Michezo