NA MWANDISHI DIRAMAKINI
BODI ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) imeufungia tena Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani baada ya kubaini bado haukidhi vigezo vya mechi za Ligi Kuu ya NBC.
Aidha,kufuatia taarifa hiyo, klabu ya Ruvu Shooting ambayo ilikuwa ikiutumia kama uwanja wake wa nyumbani italazimika kuhamia uwanja wa Uhuru uliopo jijini Dar es Salaam.
Kamati ya leseni za klabu itaukagua uwanja huo mara baada ya kukamilika kwa marekebisho hayo ili kujiridhisha kuwa unafaa kuendelea kutumika kwa michezo ya ligi.
Aidha,bodi inaendelea kuzikumbusha klabu zote kuhakikisha viwanja vyao vya nyumbani vinakuwa katika hali nzuri wakati wote kwani viwanja ambavyo vitakosa sifa vitafungiwa mara moja.