Gari la abiria lagonga treni jijini Dar es Salaam, wawili wafariki, sita wajeruhiwa

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

UONGOZI wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) umethibitisha kutokea kwa tukio la ajali lililotokea Januari 19, 2022 maeneo ya Banana jijini Dar es Salaam katika kivuko cha reli na barabara, ambapo gari la abiria aina ya ‘Coaster’ lenye namba za usajili T701 CKD linalofanya safari kati ya Tandika na Mbezi limegonga treni.
"Ajali imetokea majira ya saa 11:10 jioni na imehusisha treni ya mjini inayotoa huduma ya usafiri wa abiria kati ya Kamata na Pugu jijini Dar es Salaam, katika ajali hii majeruhi ni abiria 6 waliokuwa wakisafiri na basi ambapo wanawake ni watatu na wanaume watatu na kuna vifo vya wanawake wasili, majeruhi wote wamepelekwa Hospitali ya Amana kupatiwa matibabu.

"Dereva wa basi alitahadharishwa kwa kupigiwa honi na dereva wa treni, hakuzingatia na hata aliposimamishwa na mshika bendera dereva wa basi aliamua kukatiza reli na kupelekea ajali.

"Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania unaendelea kusisitiza Umma kuwa makini na kufuata Sheria na taratibu zinazoonesha alama zilizopo katika vivuko vya reli na barabara na dereva anapokaribia makutano anapaswa kupunguza mwendo na kusimama umbali wa mita 100 kuhakikisha endapo njia ni salama ili kuendelea na safari;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news