MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema jukumu kubwa la vyuo vikuu ni kusaidia kutatua matatizo ya jamii, kwa kufanya tafiti ili kutoa mwangaza na muelekeo wa maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Mheshimiwa Othman ametoa wito kwa vyuo vikuu vya Zanzibar kufuatilia kwa karibu maeneo mengine ya kupewa kipaumbele cha utafiti kama yalivyoainishwa katika Agenda ya Utafiti ya Zanzibar (Zanzibar Research Agenda).Soma kwa kina hapa>>>
“Hapa tunajifunza dhima na jukumu la kila chuo kikuu kuzingatia umuhimu wa kufanya tafiti zenye tija, ili kuyakabili matatizo sugu yanayokabili jamii na hasa nchi zetu ndani ya Bara la Afrika,”amesema Mheshimiwa Othman.