NA MWANDISHI MAALUM
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amefiwa na kaka yake Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Gerald Mpango. Askofu Gerald Mpango amefariki tarehe 19 Januari 2022 Jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Enzi za uhai wake Askofu Gerald Mpango alihudumu katika kanisa la Anglikana Dayosisi ya Magharibi ya Tanganyika ( Diocese of Western Tanganyika)
Mazishi ya Askofu Mstaafu Gerald Mpango yanatarijiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 22 Januari 2022 wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.

Mazishi hayo yatatanguliwa na ibada ya kuaga mwili wa marehemu itakayofanyika katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano lililopo Posta Jijini Dar es salaam siku ya Ijumaa tarehe 21 Januari 2022.

Baadaye mwili utasafirishwa kwenda mkoani Kigoma kisha kufuatiwa na Ibada ya kuaga mwili huo katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Andrea Kasulu Kigoma.
Tags
Habari