Mamia wajumuika na Makamu wa Kwanza wa Rais katika maziko ya kaka yake

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman jioni ya leo ameungana na wananchi na viongozi mbalimbali wa kiserikali,dini na kisiasa, katika maziko ya kaka yake marehemu Mwalimu Said Masoud Othman.
Marehemu Mwalimu Said Masoud, alifariki jana usiku katika hospitali ya rufaa ya Mnazi mmoja kisiwani Unguja, alikolazwa kwa matibabu siku mbili zilizopita na kuzikwa kijijini kwao Masipa Pandani, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Awali Mhe. Othman aliungana na waumini mbalimbali wa kiislamu katika ibada ya sala na kumuombea dua marehemu.
Mwili wa marehemu Mwalimu Said ulisafirishwa mapema leo asubuhi na kuwasili kijijini kwao majira ya saa tatu asubuhi.

Marehemu mbali na kuwa mwalimu katika Skuli mbalimbali Kisiwani Pemba ikiwemo Shengejuu, Pandani na Finya pia aliwahi kuwa Afisa Michezo na Afisa Utumishi katika Wizara ya Elimu Chake Chake Pemba.
Marehemu amefariki akiwa na umri wa miaka 63 na ameacha kizuka mmoja na watoto tisa.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema pema peponi. Amen

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news