Mbunge Mrisho Gambo aendelea kuwapa tabasamu watu wenye ulemavu

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MBUNGE wa Jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo amewakumbuka walemavu kwa mara nyingine kwa kuratibu utoaji wa viti mwendo na bima za afya ambapo Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Vijana,Ajira na watu wenye Ulemavu, Prof.Joyce Ndalichako amevikabidhi kwa walemavu katika jimbo hilo huku akisema kuwa serikali imetenga kiasi cha sh.bilioni 5.4 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni 50 ya watu wenye ulemavu pamoja na ununuzi wa vifaa visaidizi katika vyuo vikuu na sekondari.Akizungumza wakati wa kukabidhi visaidizi hivyo, Profesa Ndalichako alisema kuwa fedha hizo ni za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi uviko 19 ambapo zitaweza kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu kwa jamii pamoja na watu wenye ulemavu kwa kupata huduma zilizo bora. 

“Serikali imeanzisha huduma za afya tembezi lengo ni kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata huduma kama chanjo lakini pia ramani za shule pamoja na majengo yake yaliyojengwa hivi karibuni yamezingatia mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu lakini pia inaendelea kutekeleza mikataba mbalimbali ya kitaifa,kimataifa pamoja na kuandaa sera kanuni na miongozo katika kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki zao,”alisema Prof.Ndalichako. 

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Mrisho Gambo alisema jiji la Arusha lina jumla ya watu wenye ulemavu wapatao 1009 kati ya hao wanawake 440 na wanaume 569 ambao wana ulemavu wa aina mbalimbali ambapo ofisi yake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali waliona wayatambue makundi hayo ya watu ulemavu pamoja na kutambua changamoto zao na kuweza kuzitatua. 

“Baada ya kugundua kuna watu wenye ulemavu ambao wanachangamoto za matibabu ikiwa kw mwaka jana walitoa kadi za bima 100 sambamba na viti mwendo hivyo kutokana na changamoto za uhitaji zaidi ikabidi waendelee kuwapa bima watoto wote waliochini ya umri wa miaka 18 muda wa ndani ya miaka mitano,”alisema Mbunge huyo. 

Mbunge huyo alisema kwa watu wenye ulemavu wanaohitaji miguu ya bandia wapatao 117 ambao walishapimwa hivyo taratibu zinaendelea za kuikamilisha na ikikamilika watapatiwa. 

“Mheshimiwa waziri tulikuwa tunaomba kuna baadhi ya majengo hayana miundombinu rafiki kwa ajili ya watu wenye ulemavu kwani kuna baadhi ya maeneo wakifika watu hawa hufikia nje na kushindwa kupata huduma kama watu wengine,”alisema Gambo. 

Aidha alisema kupitia ofisi ya mbunge kwa kusbirikiana na madau kutoka granmelia hoteli wataonyesha mafano wa ujenzi wa choo cha kisasa cha watu wenye ulemavu katika shule ya msingi kaloleni. 

Mratibu wa huduma za viti mwendo kutoka CCBRT wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro,Neophita Lukilingi alisema vifaa tiba hivyo ni vya gharama ambapo watu wenye ulemavu pekee hawawezi kumudu hivyo wanaomba wadau mbalimbali kujitokeza katika kuwasaidia watu wenye ulemavu. 

“Vile vile tunaiomba serikali itusaidie kuongeza vifaa tiba kwa watu wenye ulemavu ili waweze kuwa na maisha bora kama watu wengine,”alisema Mratibu huyo. 

Mkurugenzi mtendaji wa Asasi kilele inayojishughulisha na kilimo cha horticulture (TAHA),Jackline Mkindi alisema hafla hiyo imelenga kugusa wati wenye mahitaji maalumu kwani mara nyingi wamekuwa wakisahau katika jamii kwa kuleta maendeleo shirikishi kwa Taifa wapo watu muhimu. 

“Napenda kutoa rai kwetu sisi wadau wa maendeleo kuendelea kushirikiana na ofisi ya mbunge wetu juu ya mambo mazuri anayoyafanya mbunge Gambo katika kuyaunga mkono kwa lengo hasa kuleta maendeleo,”alisema Mkindi. 

Nao baadhi ya wanufaika wa vifaa hivyo wameshukuru ofisi ya mbunge kwa upendo na uzalendo aliowaonyesha watu wenye ulemavu wa wilaya hiyo kwani sio kitu rahisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news