Miradi ya maji yaendelea kutekelezwa kwa kasi Singida

NA MWANDISHI DIRAMAKINI 

SERIKALI kupitia bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2021-2022 imetenga jumla ya shilingi milioni 316 Kijiji cha Mitula, shilingi milioni 500 Kijiji cha Mwighaji huku milioni 565 zikitokana na Mpango wa Serikali kupitia Fedha za Mapambano dhidi ya UVIKO-19 zikielekezwa Kijiji cha Migugu kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji wilayani Singida. 

Tayari zoezi la usambazaji vifaa kwa ajili ya kukamilisha miundombinu ya maji limeanza kutekelezeka kwa kasi na ufanisi mkubwa.Meneja wa Wakala ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Singida, Athuman Abdul Mkalimoto amesema kuwa, jumla ya miradi minne itatekelezwa kukamilisha huduma maji katika Wilaya ya Singida ambapo mradi wa Ughandi ‘B’ umeshafikia asilimia 75 na miradi mingine inaendelea kutelezwa kuanzia mwezi huu wa Januari 2022. 

“Katika kutekeleza bajenti ya mwaka wa fedha 2021-2022 tumepanga kutekeleza miradi mikuu minne. Mradi wa kwanza ni wa Mighaji wenye thamani ya milioni 500, miradi wa mipili ni wa Kijiji cha Migugu wenye thamani ya milioni 565 kupitia fedha za UVIKO mpaka sasa mkandarasi ameshapatikana, mradi mwingine ni ule wa Ughandi B umeshafikia asilimia 75,"amesema Mkalimoto. 

Ameongeza kuwa, mradi wa Kijiji cha Mitula chenye wakazi zaidi ya 2,000 sasa umeanza utekelezaji ambapo zoezi la usambazaji wa mitambo ya maji imepokelewa ambapo kukamilika kwa mradi huo utawasaidia wakazi wa kijiji hicho. 

“Tunashukuru sana serikali tumepokea mabomba yatakayokamilisha mradi wa maji katika kijiji hiki ya Mitula itatusaidia kukamilisha kwa haraka mradi huu na kuwanufaisha wananchi, tutahakikisha mradi huu unakamilika kabla ya mwezi wa tano,"amesema.

Mhandisi wa RUWASA Wilaya ya Singida, Joel Kibusi amesema uwepo wa miradi ya maji ni fursa kwa wakazi wa kijiji husika kujipatia kipato kwa kushiriki katika kazi za uchimbaji wa mtaro na utandazaji wa mitambo na kuwataka kuvitunza vyanzo vya maji . 

“Mtu atoke hapa aende achukue Wasukuma Shinyanga kweli? Wakati kuna vijana wenye nguvu, kwa hiyo nawaomba wananchi wa hapa hasa vijana na utakapotumika unalipwa, niwaombe sana mazingira yenu muyatunze kuna sehemu tunajenga kituo cha maji siku tunakwenda kukagua tunakuta kuna mtu kashusha mzigo hadi tunaoneka hatuna kitu,”amesema Mhandisi Kibusi. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news