NA MWANDISHI DIRAMAKINI
MSANII wa Bongo Fleva nchini na aliyewahi kuwa Diwani wa Mwanga Kaskazini (ACT-Wazalendo) Manispaa ya Kigoma Ujiji, Clayton Chipando maarufu Baba Levo ametunukiwa udaktari wa heshima.
Udaktari huo ametunukiwa na College of Health and Allied Sciences cha jijini Mwanza ambapo cheti chake kinabainisha kuwa, heshima hiyo imejikita katika afya,siasa,sanaa na burudani.
Msanii huyo ambaye pia ni mtangazaji wa Wasafi FC ameyabainisha hayo kupitia cheti alichoambatanisha katika ukurasa wake wa kijamii.