NA MWANDISHI DIRAMAKINI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi alikuwa mgeni rasmi katika burudani ya muziki wa Taarabu asilia, iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya maadhimisho ya kusherehekea miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Msanii Profesa Mohammed Elias akito burudani wakati wa Taarab rasmi ya Kikundi cha Taifa cha Zanzibar akiimba wimbo wa Nimesafi Moyo,wakati wa hafla ya Taarab ya kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni jijini Zanzibar.
Hafla hiyo imefanyika Januari 12,2022 katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-wakil, Kikwajuni jijini Zanzibar, ambapo magwiji wa sanaa ya muziki wa Taarabu asilia kutoka Kikundi cha Taifa Zanzibar, walionyesha umahiri wao katika kucharaza nyuzi na kughani nyimbo mbalimbali na kukonga nyoyo za mashabiki wa sanaa hiyo kutoka mikoa yote ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana na Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe.Tabia Maulid Mwita, alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni kuhudhuria hafla ya Taarab rasmi ya kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa amesimama wakati ukipingwa wimbo wa Taifa wa Zanzibar na Kikundi cha Taifa cha Taarab Zanzibar, kabla ya kuaza kwa Taarab rasmi ya kusherehekea maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, kushoto kwa Rais ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na (kulia kwa Rais ni Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi na Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe.Tabia Maulid Mwita, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni jijini Zanzibar.
Wasanii wa Kikundi cha Taifa cha Taarab Zanzibar wakipiga wimbo wa Taifa wa Zanzibar kabla ya kuaza kwa Taarab rasmi ya Maadhimisho ya kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe Dkt.Hussein Ali Mwinyi na kushoto kwake ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na kulia kwa Rais ni Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe.Tabia Maulid Mwita, wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar, Bi.Fatma Hamad Rajab, akisoma ratiba ya Taarab Maalum ya kusherehekea Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni jijini Zanzibar.
Msanii Nassor Hussein akiimba wimbo wa kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi, wakati wa hafla ya Taarab Rasmi ya kusherehekea maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, wakati Kikundi cha Taifa cha Taraab Zanzibar wakitoa burudani, katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakili Kikwajuni jijini Zanzibar.
Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi akijumuika na wananchi katika Taarab Maalum ya Kikundi cha Taifa cha Zanzibar na (kulia), Mhe. Asha Abdalla Juma , katika taarab rasmi ya kusherehekea maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni jijini Zanzibar.
Katika burudani hiyo nyimbo mbalimbali zilizopata kuvuma na kupendwa kutoka kwa watunzi wabobezi na waimbaji nguli wa sanaa hiyo zilipata fursa ya kuimbwa na kuibua vifijo na nderemo.
Nyimbo ya kwanza ambayo ilifungua pazia la burudani hiyo, ilikuwa ni ile iliyoendana na maudhui ya sherehe hizo, ambapo Mwimbaji nguli Al-anisa Fatma Dawa alighani kwa ustadi mkubwa na kuwafanya watazamaji kuinuka kwenye viti na kumtunza.
Aidha, kumalizika kwa nyimbo hiyo, kulitoa fursa kwa mwimbaji mahiri Al - anisa Hilda Mohamed kughani nyimbo maarufu na iliowahi kupata sifa kubwa hapa Zanzibar, ijuilikanayo kwa jina la ‘Nisubiri hadi lini’.
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe.Mgeni Hassan Juma na kushoto ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, wakifuatilia hafla ya Taarab Rasmi ya Kikundi cha Taifa cha Zanzibar, kusherehekea maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni.
Msanii wa Kikundi cha Taifa cha Taarab Zanzibar, Amina Abdalla akiimba wimbo wa Kibali wakati wa Taarab rasmi ya kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni jijini Zanzibar.
Kadri muda ulivyosonga, ndivyo burudani hiyo ya taarabu iliendelea kunoga na kuufanya usiku huo kuwa maalum kwa wapenzi na mashabiki wa sanaa hiyo, hususan pale zilipoimbwa nyimbo maarufu kama vile, Cheo chako, Kibali, Kweli ninae, Mpewa hapokonyeki, Lulu, Ubinafsi na choyo, Lipi nilopenda kwako na kuhitimishwa na nyimbo ya Wahoi.
Nyimbo nyingine zenye mnasaba na maudhui ya sherehe hizo ambazo zilipata nafasi ya kuimbwa na kuibua shwangwe kubwa, ni pamoja na ile ya kumpongerza Dk. Mwinyi kwa Uongozi wake, ilioimbwa na msanii nguli Nassor Hussein.
Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi akitabasamu na kufurahia jambo wakati wa hafla ya Taarab Rasmi ya kusherehekea maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, wakati Kikundi cha Taifa cha Taarab Zanzibar wakitoa burudani katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni jijini Zanzibar na kulia ni Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe.Tabia Maulid Mwita.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akifuatila hafla ya Taarab Rasmi ya kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar iliyofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni jijini Zanzibar na kushoto kwa Rais ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe.Hemed Suleiman Abdulla.(Picha na Ikulu).
Katika hafla hiyo, ambapo Rais Dkt. Mwinyi aliambatana na Mama Mariam Mwinyi, watazamaji na mashabiki wa sanaa ya taarabu asilia walikoshwa na kupata kile mioyo yao inapenda, baada ya kuwashuhudia wasanii nguli kama vile Ustadh Idd Sued (mpendwa na wengi) na Profesa Mohamed Elias wakiendelea kuimba kwa sauti ile ile iliyozoeleka kwa miaka na dahari na kuthibitisha ule usemi wa ‘vya kale ni dhahabu’.
Viongozi mbalimbali wa Kitaifa, akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Hemed Suleiman Abdalla walishiriki.