Pia imeezua nyumba 36 za makazi ya watu pamoja na kuharibu mazao mbalimbali mashambani kutokana na maafa hayo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Hassan Mwinyi Kondo ambae aliambatana na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Ramadhani Possi, Diwan wa Kata ya Lugoba, Rehema Samwel na Mwenyekiti wa Huduma za Jamii, Juma Mpwimbwi walifika katika Shule ya Msingi Makombe kuona uharibifu uliojitokeza. “Tumekuja hapa kujionea maafa,tumejionea, hivyo kubwa zaidi mikakati ya ziada ni kuhakikisha hali ya awali inarudi, halmashauri yetu imejipanga na tumeagiza kufanywe tathmini haraka,“amesema Mwinyikondo.
Diwani wa Kata ya Lugoba, Rehema Mwene amesema, jambo hilo linahitaji usimamizi wa haraka,kwani wananchi wameshtushwa na kama kata wamejipanga kuangalia namna ya kusaidia waliopata janga hilo.
Mkuu wa shule hiyo,Norah Mtabwa alieleza,darasa la saba wamehamishiwa darasa la awali wakitoka na darasa la pili wanapishana na darasa la kwanza na wakati kadhia hiyo ikitokea bahati nzuri ilikuwa muda wa kutoka shule.
Afisa Elimu Msingi Chalinze, Mariam Kihiyo amefafanua kuwa, madarasa yaliyoezuliwa kutokana na mvua ni mawili na hakuna watoto wanaokosa masomo kwa kuwa wanapokezana ikiwemo wanafunzi wa madarasa yaliyoezuliwa.