Naibu Waziri wa Madini Dkt.Kiruswa atembelea GST, awapongeza kwa kazi nzuri

NA MWANDISHI MAALUM

NAIBU Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa jana Januari 20 , 2022 ametembelea Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali za taasisi hiyo.
Dkt.Kiruswa alifika katika ofisi za GST na kusaini kitabu cha wageni na kuanza ziara ya kutembelea Kurugenzi za Taasisi kwa lengo la kujifunza na kuangalia jinsi shughuli za taasisi zinavyofanyika.
Sehemu alizotembelea ni pamoja na Makumbusho ya Miamba na Madini, Maabara ya Madini, Sehemu ya uzalishaji wa ramani za jiosayansi pamoja na eneo maalum la utunzaji wa taarifa za Taasisi (Archives).
Baada ya ziara katika maeneo hayo, Mtendaji Mkuu wa GST, Dkt. Mussa Budeba alitoa wasilisho maalum kwa Naibu Waziri juu ya historia ya GST pamoja na kazi mbalimbali zilizofanywa na zile ambazo zinaendelea kutekelezwa kupitia wataalam wake.
Baada ya kumalizika kwa wasilisho maalum, Naibu Waziri alipata fursa ya kukaa kikao na Menejimenti nzima ya GST na kuipongeza kwa kazi nzuri zinazofanywa na GST katika kuendeleza Sekta ya Madini nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news