Orodha ya Mawaziri na Manaibu Waziri waliopumzishwa na Rais Samia

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametimiza ahadi yake ya kuendelea kuachilia orodha ya viongozi ambao anaamini watamsaidia muda wowote kutekeleza mipango ya Serikali ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Januari 4, 2022 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea taarifa ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19, Mheshimiwa Rais Samia alionyesha dhamira ya kufanya mabadiliko ya haraka ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji katika Serikali anayoiongoza.

Mheshimiwa Rais alisema, baada ya kukaa kwenye nafasi hiyo miezi kadhaa amewasoma mawaziri na utendaji wao hivyo atatoa orodha mpya ya wateule ambao anaona watamsaidia kuwaletea wananchi maendeleo.

Katika mabadiliko madogo aliyoyafanya Mheshimiwa Rais Samia yaliyotangazwa Januari 8, 2021 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga katika Baraza la Mawaziri baadhi ya mawaziri na manaibu waziri wamepumzishwa.

Mawaziri waliopumzishwa ni aliyekuwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi na aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi.Unaweza kusoma, Orodha ya Makatibu na Manaibu Katibu Wakuu hapa>>>

Mwingine ni Geoffrey Mwambe, aliyekuwa Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo.

Kwa upande wa manaibu waziri walioachwa ni Profesa Shukurani Manya kutoka Wizara ya Madini huku nafasi yake ikichukuliwa na Dkt. Lemomo Kiruswa.Orodha kamili ya Mawaziri na Manaibu Waziri soma hapa>>>

Mwingine ni Mheshimiwa Mwita Waitara kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ambapo nafasi yake imechukuliwa na Atupele Mwakibete.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news