Uteuzi wa viongozi hawa umefanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Januari 8,2022 na wanatarajia kuapishwa Januari 10,2022 katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
Kutoka WCF
Wakati huo huo,Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ambayo ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoundwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura 263 marejeo ya mwaka 2015] na inahusu waajiri na waajiriwa wote Tanzania Bara, imetoa pongezi kwa viongozi walioteuliwa.
Lengo la Serikali kuanzishwa mfuko huu ni kushughulikia masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi waliopo katika sekta ya umma na binafsi ambao wataumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi wanazozifanya kwa mujibu wa mikataba ya ajira zao.