NA MWANDISHI DIRAMAKINI
WATU watano wakiwemo watoto wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi katika Kijiji cha Kibuye Kata ya Kumsenga wilayani Kibondo mkoani Kigoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, James Manyama amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 12 jioni ambapo mvua mkubwa iliyokuwa ikinyesha huku ikiambatana na radi ilisababisha vifo vya watoto wanne wenye umri unaokadiriwa kuwa na miaka mitano na 10 pamoja na mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 50.
Amesema, watoto hao wakiwa wanacheza chini ya mti wa mwembe walipigwa na radi na kufariki hapo hapo huku mwanamke ambaye naye alikuwa shambani akiendelea na shughuli za kilimo ambapo alikutwa na radi hiyo na kufariki.
Kamanda huyo amewataja marehemu kuwa ni Baseka Japheth (10) mwanafunzi wa darasa la tano shule ya msingi Kibuye, Goma Jeremia (5), Rock Ramadhani (5), Alam Paschal (9) na Anatolia Muhoza (50) wote wakazi wa kijiji cha Kibuye wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.