Rais Dkt.Mwinyi aelekea UAE kwa ziara ya kikazi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameondoka nchini leo kuelekea Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (U.A.E) kwa ziara ya siku tatu.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, Rais Dkt. Mwinyi aliagwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa, dini pamoja na wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla pamoja na Viongozi wengine katika uwanja wa Ndege wa Kimatafa wa Abeid Amani,wakati akiondoka nchini leo kuelekea katika nchi za falme za kiarabu kwa ziara ya Kikazi.

Ziara hiyo ya Rais Dkt. Mwinyi ni kufuatia mwaliko maalumu wa Kiserikali aliopewa na Mrithi wa Mtawala wa Abudhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi wa Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Marium Mwinyi wakiagana na viongozi wa Vikosi vya Ulinzi katika uwanja wa Ndege wa Kimatafa wa Abeid Amani Karume akiondoka nchini leo kuelekea katika nchi za falme za kiarabu katika ziara ya kikazi.

Rais Dk. Mwinyi anatarajia kuanzia ziara yake hiyo nchini Abudhabi ambako atahudhuria Maadhimisho ya wiki Maalum ya Kushajihisha Maendeleo endelevu inayoadhimishwa kila mwaka nchini humo iliyoazia tangu mwaka 2008 pamoja na kuhudhuria mkutano wa wakuu wa Nchi na Serikali mbali mbali duniani utakaofanyika huko nchini Dubai.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na wasaidizi wake katika uwanja wa Ndege wa Kimatafa wa Abeid Amani Karume akiondoka nchini leo kuelekea katika nchi za falme za kiarabu katika ziara ya kikazi akifuatana na Mkewe Mama Marium Mwinyi .(Picha na Ikulu).

Katika ziara hiyo, Rais Dk. Mwinyi amefuatana na mkewe Mama Mariam Mwinyi pamoja na viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Husein Ali Mwinyi anatarajiwa kurejea nchini Jumatano, tarehe 19 Januari 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news