Rais Dkt.Mwinyi asisitiza umuhimu wa bima kwa wananchi, wawekezaji

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema ili nchi za Kiafrika ziweze kutekeleza vyema mageuzi ya kiuchumi na kukuza ustawi wa wananchi, ni lazima kuwa na sekta na taasisi za bima imara na zinazokwenda sambamba na kasi ya maendeleo ya Sayansi na Teknolojia katika karne ya 21.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizindua kitabu kinachuzungumzia mabadiliko ya tabia nchi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Bima na Hifadhi ya Jamii Afrika uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahr Mbweni Zanzibar na kushoto kwa Rais ni Waziri wa Nchi Ofisi Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe.Jamal Kassim Ali na kulia kwa Rais ni Naibu Kamishna wa Bima Tanzania (TIRA),Bi. Khadija Said. (Picha na Ikulu).

Mheshimiwa Dkt.Mwinyi amesema hayo Januari 26,2022 katika ufunguzi wa Mkutano wa Bima kwa nchi za Afrika, uliofanyika katika Hoteli ya Madinat Bahr uliopo Mbweni jijini Zanzibar.
Amesema katika kujenga na kuendeleeza uchumi wa kisasa, uwepo wa mfumo, sheria na taratibu madhubuti za uendeshaji wa shughuli za Bima ni muhimu ili kuwapa wawekezaji imani na uhakika wa usalama wa mitaji wanayotaka kuwekeza. 

Amesema, pamoja na kuwepo maendeleo katika sekta hiyo, Afrika inapaswa kuendelea kuimarisha sekta hiyo ili iweze kuyafikia makundi yote ya wannachi yanayojishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi, hususan katika sehemu za vijijini.

Pia amesema wananchi wengi wamekuwa wakiendesha shughuli zao bila ya kuwa na kinga ya bima, hivyo akatumia fursa hiyo kutoa wito kwa mataifa ya Afrika kuwaelimisha wananachi wao umuhimu wa kuwa na bima,pamoja na kutaka bima hizo zitolewe kwa gharama nafuu na kwa wakati muafaka, hususan pale wananchi wanapopata misukosuko ya kiuchumi.  Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Bima na Hifadhi ya Jamii Afrika, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia na kuufungua mkutano huo uliofanyika katika ukumbi Hoteli ya Madinat Al Bahr Mbweni Zanzibar 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akionesha Kitabu kinachuzungumzia Mabadiliko ya Tabia Nchi, baada ya kukizindua wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Bima na Hifadhi ya Jamii Afrika uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahr Mbweni Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe.Jamal Kassim Ali na (kulia kwa Rais) Naibu Kamishna wa Bima Tanzania (TIRA),Bi. Khadija Said.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizindua tovuti ya “Africa College of Insurance and Social Protection” (ACISP).www.acisp.africa,www.acisp.net, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Bima na Hifadhi ya Jamii Afrika “Africa Insurance Retreat” uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahr Mbweni Zanzibar.

 Rais Dkt.Mwinyi akaelezea furaha aliyonayo kutokana na maudhui ya mkutano huo yanayosisitiza umuhimu wa kuongeza juhudi katika kufikisha huduma za Bima kwa wananchi wengi zaidi ili kukuza sekta hiyo, ikiwemo Bima ya Afya, Bima ya Maisha, pamoja na kuwajengea uwezo watendaji.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inalenga kuanzisha Bima ya Afya, ikiwa ni hatua ya kuimarisha utoaji wa huduma hizo kwa wananchi, ambapo kwa kipindi kirefu ilishindwa kukidhi haja kutokana na kutegemea Bajeti yake kwa asilimia mia moja. 

Aidha, alitumia fursa hiyo kuzialika Kampuni mbali mbali za Bima Barani Afrika kuja kuwekeza Zanzibar ili kuendeleza uchumi wa Buluu, akibainisha kuwepo fursa nyingi za kiuchumi . 

“Hatutopenda wawekezaji tunaowavutia kuja kuwekeza Zanzibar kwenye Bandari za kisasa, kwenye uvuvi, kwenye mafuta na gesi, wanakata bima zao nje, ni vyema tukahakikisha bima zao wanakata hapa hapa nchini,”amesema. 
Dkt.Mwinyi amewahakikishia washiriki wa mkutano huo kuwa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na kampuni mbalimbali za bima Barani Afrika ili kuhakikisha malengo ya kufikisha huduma bora za bima kwa wananchi wote mjini na vijijini zinafikiwa. 

Nae, Waziri wa Nchi (OR) Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali amesema ni wakati mwafaka kwa washiriki wa mkutano huo kujadili umuhimu wa shughuli za Bima ya Afya Barani humu, kuambatana na Azimio la Abuja (Abuja Declaration). 

Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya Nchi, (OR) Fedha na Mipango Dkt.Malik Akil alisema Serikali inaamini kuna kazi kubwa inayopaswa kufanyika ili kuhami rasilimali za Bahari na zile zenye mnasaba na hizo ili kuiwezesha Zanzibar kufikia azma ya kuimarisha uchumi wa Buluu. 
Mapema, Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Khadija Issa Said alisema pamoja na mafanikio makubwa yaliopatikana katika uendeshaji wa Sekta ya Bima Afrika na hususan Tanzania, kuna changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta hiyo, ikiwemo uelewe mdogo wa wananchi, hususan walio vijijini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news