Rais Samia ateua viongozi TANTRADE, TTCL na Tume ya TEHAMA

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 29, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu.
Walioteuliwa na Mheshimiwa Rais Samia ni Profesa Ulingeta Mbamba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Profesa Mbamba anachukua nafasi ya Dkt.Ng'wanza Kamata Soko aliyemaliza muda wake.

Profesa Mbamba ni Profesa Mshiriki na Amidi wa Shule Kuu ya Biashara, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Pili, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Bi.Zuhura Sinare Muro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Bi.Muro ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ushauri Elekezi ya Kazi Services Limited na Mkufunzi wa muda katika Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute), Dar es Salaam.

Tatu, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Profesa Leonard James Mselle kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya TEHAMA.

Profesa Mselle ni Mhadhiri, Rasi Ndaki ya Sayansi na Kompyuta na Elimu Angavu, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Taarifa hiyo imeeleza kuwa, uteuzi huo umeanza leo Januari 29, 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news